Simba kucheza mechi saba kwa wiki mbili ligi kuu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Apr 2019
Simba kucheza mechi saba kwa wiki mbili ligi kuu

Keshokutwa Jumatano Simba inarejea rasmi kwenye mchakamchaka wa ligi kuu ya Tanzania Bara kwa kuikabili Coastal Union katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Mkwakwani mkoani Tanga

Kutokana na muda mchache uliobaki kabla ya ligi hiyo kumalizika mwezi ujao, Simba inakabiliwa na ratiba ya kucheza mfululizo ambapo katika kipindi cha wiki mbili itashuka dimbani mara saba

Baada ya mchezo dhidi ya Coastal Union April 17, mchezo utakaofuata ni dhidi ya Kagera Sugar utakaopigwa mkoani Kagera katika uwanja wa Kaitaba April 20

April 23 Simba itakuwa Mwanza kuchuana na Alliance Fc katika mchezo utakaopigwa uwanja wa CCM Kirumba kisha kurudi dimbani hapo April 26 kumenyana na KMC

Siku mbili baadae April 28 Simba itaelekea mkoani Mara kuikabili Biashara United kabla ya kuelekea mkoani Mbeya ambako May 01 itacheza na Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine kisha kurejea tena dimbani hapo May 03 kuumana na Mbeya City

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’