Aussems hesabu zote ligi kuu, awataka mashabiki wa Simba wasihuzunike

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Apr 2019
Aussems hesabu zote ligi kuu, awataka mashabiki wa Simba wasihuzunike

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema hatua waliyofika msimu huu katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika sio haba na mashabiki wa timu hiyo wana kila sababu ya kutembea kifua mbele

Simba imetolewa hatua ya robo fainali ya michuano hiyo juzi kwa kufungwa mabao 4-1 na TP Mazembe

Hata hivyo kufika hatua hiyo ni mafanikio makubwa kwa Simba ambayo ilijiwekea malengo ya kutinga angalau hatua ya makundi

Aussema amesema walipoteza mchezo dhidi ya TP Mazembe kwa kuwa wapinzani wao walijipanga na kupeleka mashambulizi ya mara kwa mara langoni kwao na hatimaye walifanikiwa kurejesha bao walilofunga mapema na kufunga mengine matatu ambayo yaliwakatisha tamaa wachezaji wake.

"Haikuwa mipango yetu, lakini tulistahili kusonga mbele, kwangu kuingia hatua ya nane bora ilikuwa nafasi kubwa sana na wote tulikuwa na nafasi sawa, ila uzoefu na ubora wa vikosi vyetu ndio umechangia matokeo haya, naamini msimu ujao tutakuwa imara na bora zaidi," alisema Aussems.

Mbelgiji huyo amesema sasa wanaelekeza nguvu zao kwenye ligi kuu kuhakikisha wanatetea ubingwa ili kupata nafasi ya kshiriki michuano hiyo mwakani.

Simba imeelekea mkoani Tanga ambapo keshokutwa Jumatano itaivaa Coastal Union

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’