Balozi wa Tanzania nchini DR Congo, Luteni Jenerali (Mstaafu) Paul Mella mapema leo amekutana na wachezaji wa Simba ambapo amewataka kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye mchezo wa leo kwani ushindi sio tu muhimu kwa klabu bali kwa Taifa
Muda mchache ujao Simba itashuka uwanja wa TP Mazembe kuwakabili wenyeji wao katika mchezo wa pili wa robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Katika mchezo huo unaotarajiwa kupigwa saa tisa kwa muda wa Congo na saa kumi Tanzania, Simba inahitaji ushindi au matokeo ya sare ya mabao ili kuweza kufuzu hatua ya nusu fainali


ADVERTISE HERE