Zana, Okwi wapewa kazi maalum Congo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Apr 2019
Zana, Okwi wapewa kazi maalum Congo

Wachezaji Zana Coulibaly na Emmanuel Okwi wamepewa kazi maalum huko Lubumbashi kuhakikisha wanawaondoa TP Mazembe kwenye mechi ya marudiano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kesho Jumamosi

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesisitiza kwamba kikosi chake kitakachocheza wikiendi hii kitakuwa na Sapraizi za kumwaga na Emmanuel Okwi guu lake litafanya maajabu.

"Okwi hatukutaka ajitoneshe katika mchezo huo kutokana na kuwa mechi nyingine ya marudiano tutakayocheza wikiendi hii na kweli tunashukuru alipoingia alionyesha utofauti mkubwa.

"Baada ya kumuona kwenye mazoezi ya siku hizi mbili tuliyoyafanya ni matarajio yangu kumuona akiongeza kitu cha tofauti katika mchezo wetu wa marudiano dhidi ya Mazembe," alisema Aussems na kusisitiza kikosi chake kitakuwa na mabadiliko makubwa.

Naye beki aliyen'gara kwenye mchezo uliopita Zana Coulibaly amewatoa hofu mashabiki kuwa wana nafasi ya kupata matokeo ugenini na kutinga hatua ya nusu fainali

"Mashabiki hawatakiwi kuwa na wasiwasi kwa kuwa tunajua tutachoenda kukifanya kwenye mchezo wa marudiano," Zana amenukuliwa na Salehjembe

"Kila timu bado ina nafasi ya kushinda kwa sababu kwenye mchezo wa kwanza hakuna aliyeweza kumfunga mwenzake"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
22h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’