Ni mchezo wa jasho na damu - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Apr 2019
Ni mchezo wa jasho na damu - Manara

Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara amesema kikosi cha timu hiyo kinatarajiwa kuondoka mapema kesho Ijumaa kuelekea DR Congo tayari kwa mchezo wa pili wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya TP Mazembe

Manara amesema Simba inakwenda Congo kupambana na watahakikisha wanaiwakilisha vyema nchi kwa kupata matokeo mazuri katika mchezo huo utakaopigwa keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa TP Mazembe

Amesema wachezaji wa Simba wako tayari kuandika historia nje ya nchi

"Tunakwenda kesho kibingwa tukiwa hatuna cha kupoteza ila tunawaahidi jasho jingi litamwagika kuipigania Simba na nchi Jumamosi," amesema Manara

"Hatuogopi lolote toka Mazembe pamoja na kuwapa heshima yao kama klabu kubwa"

"Wachezaji wetu wapo tayari kuionyesha Afrika ubora wao na ukubwa wa Simba. Tuombeeni tufike salama na turejee salama kifua mbele"

Simba inakwenda Congo kwa usafiri wa ndege maalum ya kukodi na itarejea nchini Jumamosi jioni baada ya mchezo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’