Makundi AFCON 2019 kupangwa kesho

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
11 Apr 2019
Makundi AFCON 2019 kupangwa kesho

Droo ya upangaji wa makundi ya fainali za (AFCON 2019) inatarajiwa kufanyika kesho Aprili 12 jiji la Cairo nchini Misri ambapo Tanzania imewekwa kwenye chungu cha nne ikiwa pamoja na mataifa ya Mauritania, Namibia, Kenya, Benin na Madagascar.

Vyungu hivyo vimepangwa kwa mujibu wa viwango vya soka vya CAF, ambapo makundi sita yanatarajiwa kuundwa, kila kundi likiwa na timu nne na timu zilizo kwenye chungu kimoja hazitakutana kwenye kundi moja.

Kati ya mataifa 24 yaliyofuzu fainali hizo, ni mataifa matatu ambayo yamefuzu kwa mara ya kwanza katika historia yake ambayo ni Burundi, Mauritania na Madagascar

Hii ni mara ya kwanza kwa Afrika Mashariki kuingiza timu nne kwa wakati mmoja kwenye michuano hiyo, ambazo ni Tanzania, Uganda, Kenya na Burundi.

Hafla ya upangaji makundi inatarajiwa kuanza saa tatu usiku kwa saa za Afrika Mashariki ambapo Rais wa TFF Wallace Karia ataiwakilisha Tanzania

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
7h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
9h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
10h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
16h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’