Mo ameahidi makubwa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
4 Dec 2017
Mo ameahidi makubwa Simba
Baada ya kushinda Zabuni ya uendeshaji wa klabu ya Simba, Mfanyabishara Mohammed Dewji amesema anakusudia kufanya mapinduzi katika uwendeshaji wa klabu hiyo kuifanya kuwa klabu tajiri zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Mo alitangazwa kushinda zabuni ya uendeshaji wa klabu ya Simba jana kwenye Mkutano Mkuu wa klabu hiyo uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Baada ya kutangazwa, MO ametoa ahadi ya kujenga viwanja viwili ndani ya muda mfupi na akasisitiza, usajili watakaoufanya kila mwaka, hautapungua kiasi cha Sh. 1 bil.

Akitoa ahadi hiyo katika hotuba yake ya shukrani baada ya kutangazwa kama mshindi wa zabuni na Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Thomas Mihayo, Mo alisema ni aibu kwa Simba kutokuwa na uwanja wake wa mazoezi na mechi.

"Nitahakikisha Simba inakuwa na uwanja wenye nyasi za asili lakini pia nitajenga uwanja mwingine wenye nyasi bandia," alisema Mo.

Katika hatua nyingine, Mo alitoa angalizo kwa wachezaji wa timu hiyo kujituma huku akiahidi fungu kubwa la fedha katika bajeti ya usajili.

"Wachezaji wa Simba ni lazima watambue thamani ya jezi ya hii klabu hivyo wanapaswa kujituma. Pia nitahakikisha kiasi kidogo cha fedha ambazo tutakuwa tunazitumia kwenye usajili ni Sh. 1 bil," aliongeza Mo
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
4h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
10h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
13h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
16h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’