Kiungo wa Simba Jonas Mkude jana alitoa fedha taslim Tsh laki tano kuchangia matibabu ya beki wa zamani wa Simba na timu ya Taifa, Alphonce Modest
Mkude alikabidhi kiasi hicho cha fedha kwa chama cha wanasoka wa zamani ambacho pia kilitoa Tsh laki saba kusaidia matibabu ya mkongwe huyo anayesumbuliwa na maradhi kwa muda mrefu
Enzi zake Modest alikuwa beki mahiri wa kushoto ambapo aliitumikia Simba kwa mafanikio makubwa mwishoni kwa miaka ya 90
Tukio linalomuhusu ambalo litabaki katika kumbukumbu ni lile la mwaka 1998 ambapo Simba iliwaazima Yanga beki huyo ili awasaidie kwenye michuano ya ligi ya mabingwa hatua ya makundi
ADVERTISE HERE