Bocco asilaumiwe kwa kukosa penati - Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
7 Apr 2019
Bocco asilaumiwe kwa kukosa penati - Aussems

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema matokeo ya suluhu waliyopata dhidi ya TP Mazembe jana yalitokana na timu hiyo kukosa bahati na hakuna jambo jengine

Aussems amesema wachezaji wake jana walicheza kama alivyowaelekeza walitengeneza nafasi nyingi, lakini walikosa bahati

Akizungumzia tukio la nahodha John Bocco kukosa mkwaju muhimu wa penati ambayo huenda ingeiweka Simba katika mazingira mazuri ya kuibuka na ushindi, Aussems amesema Bocco hawezi kulaumiwa kwa kukosa penati kwa kuwa hiyo ni sehemu ya mchezo

"Huwezi kumlaumu mchezaji kwa kukosa penati kwani, hilo ni pigo la bahati pia," alisema

"Wachezaji wote duniani huwa wanakosa penati hivyo hapaswi kulaumiwa"

Nae msemaji wa Simba Haji Manara amewashukia baadhi ya mashabiki wa timu hiyo ambao wamemshambulia Bocco baada ya mchezo wa jana

Manara amesema Bocco ndiye mchezaji ambaye yuko katika kiwango bora zaidi katika kikosi cha Simba kwa sasa

Kwa siku za karibuni Bocco ameifungia Simba mabao mengi kwenye ligi pamoja na kutoa pasi muhimu bila kusahau amekuwa na rekodi nzuri ya kufunga mikwaju ya penati

"Kumlaumu Bocco kwa kukosa mkwaju wa penati kunasababisha na ugeni wa baadhi ya mashabiki kwenye soka," amesema Manara

"Bocco huyu ndiye anayefunga penati nyingi za Simba. Hata tulipocheza na Nkana kule Kitwe Zambia, ni Bocco aliyefunga penati muhimu ambayo baadae ilitusaidia kupata matokeo ya kuingia hatua ya makundi"

"penati ni pigo la bahati na halina mwenyewe"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
Goli la ushindi dhidi ya Fountain Gate; FT : Fountain Gate 0-1 Simba
11h ago
READ MORE β†’
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
Simba mwendo mdundo, yaichapa Fountain Gate 1-0 Tanzanite Kwaraa
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
15h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
15h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
17h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
18h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
18h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
23h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’