Mo awaita mashabiki 'kwa Mkapa' kushuhudia kipigo cha TP Mazembe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Apr 2019
Mo awaita mashabiki 'kwa Mkapa' kushuhudia kipigo cha TP Mazembe

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' amewataka mwashabiki wa Simba na wazalendo wote wa soka nchini kujitokeza kwa wingi kesho katika uwanja wa Taifa wakati mabingwa hao wa nchi wakipepetana na TP Mazembe katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ligi ya mabingwa barani Afrika

Akizungumza na waandishi wa habari mapema leo, Mo amesema kikosi cha Simba kimefanya maandalizi ya kutosha kuelekea mchezo huo, sehemu iliyobaki ni ya mashabiki kujitokeza kwa wingo uwanjani ili kuwaongezea wachezaji morali ya ushindi

"Tumejipanga vizuri sana, ari ya wachezaji wetu ni kubwa na Mungu akitujalia basi kesho tutafanya maajabu. Mimi kilichonileta hapa ni kuwaomba mashabiki wa Simba, Watanzania wajitokeze kwa wingi uwanjani," amesema Mo

"Kujitokeza kwa mashabiki kuna faida kuu mbili, moja unawaongezea nguvu wachezaji wetu na wao wanaona kuwa Watanzania wapo nyuma yao, lakini pili inawaogopesha wapinzani wetu"

Mo amesema mashabiki wa Simba wameifanya timu hiyo iandike rekodi ya kuwa timu namba moja kwa kujaza uwanja katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu

"Niwashukuru mashabiki wa Simba, niwapongeze ukiangalia takwimu za mechi za Ligi ya Mabingwa hakuna timu ambayo imejaza uwanja wake kama Simba Sports Club, Simba inaongoza kwa kujaza uwanja kwenye mechi zake"

"Nawaomba sana mashabiki ikitokea bahati mbaya ya hapa na pale, tuendelee kushabikia sio tu mpaka tukipata goli, naomba sana tubadilike kwenye hilo, tushangilie Simba tangu mwanzo hadi mwisho"

"Hapa hatushiriki tu, tunajiamini kwamba tunaweza na tunataka kwenda mbali zaidi ya hapa"

"Shabaha yetu sio tu kufanikiwa mwaka mmoja, tunataka kushinda kombe kila mwaka ili tushiriki Ligi ya Mabingwa kila mwaka, tunataka kushinda kombe la Ligi ya Mabingwa Afrika, mimi naamini uwezo tunao, tumtangulize Mungu"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
Kikosi : Fountain Gate vs Simba, NBC PL, Oct 29
1h ago
READ MORE β†’
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
Kamati ya uchaguzi Simba imesisitiza, mchakato unaendelea
1h ago
READ MORE β†’
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
Mangungu aibuka, apinga mchakato wa uchaguzi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
Tutapambana tuvuke mtoano - Barker
5h ago
READ MORE β†’
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
Matchday; Fountain Gate vs Simba, NBC PL
7h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
10h ago
READ MORE β†’
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
1d ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
1d ago
READ MORE β†’