Kagere anakitaka kiatu cha dhahabu Ligi Kuu

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Apr 2019
Kagere anakitaka kiatu cha dhahabu Ligi Kuu

Mshambuliaji Meddie Kagere ametimiza mabao 14 yanayozidi kumweka kwenye nafasi nzuri ya kufukuzana na Salim Aiyee anayeongoza chati ya ufungaji wakati Simba ikichapa Mbao kwa magoli 3-0 kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.

Kabla ya bao hilo ambalo Kagere alilifunga mnamo dakika ya 79 kwa mkwaju wa penalti, mshambuliaji huyo alikuwa amepachika mabao 13 ambayo yalikuwa ni matatu nyuma ya yale ya Aiyee wa Mwadui mwenye mabao 16 kwa sasa.

Penalti hiyo Kagere alipiga kwa ustadi mkubwa akimpoteza kipa kwa kukimbia na kusita kabla kupiga jambo lililomwacha kipa wa Mbao akiruka upande tofauti na mpira ulipoingia.

Penalti hiyo ilitokana na faulo ya beki Amimu Abdulkarim kumuangusha mshambuliaji huyo ndani ya eneo la hatari la Mbao FC.

Bao hilo la Kagere lilikuwa ni kama sukari inayopakwa juu ya keki kwani tayari Simba ilikuwa imeshajihakikishia ushindi kupitia mabao mawili ya nahodha wao John Bocco.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’