Simba vs JKT Tanzania kupigwa Jumatano

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Apr 2019
Simba vs JKT Tanzania kupigwa Jumatano

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba keshokutwa Jumatano watashuka uwanja wa Jamhuri kuikabili JKT Tanzania katika mchezo wa ligi hiyo

Licha ya kukabiliwa na mchezo wa robo fainali ligi ya mabingwa siku ya Jumamosi, April 06 dhidi ya TP Mazembe, TFF imegoma kusogeza mbele mchezo dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa April 03 2019 kama ulivyopangwa

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kwa sasa wanaelekeza nguvu zao kuelekea mchezo huo kabla ya kuanza maandalizi ya mchezo dhidi ya TP Mazembe

"Nitalazimika kubadili kikosi ili kila mchezaji apate nafasi kwani baada ya mchezo huo tutakuwa na siku mbili tu za kujiandaa kabla ya kuivaa TP Mazembe," amesema

Akizungumzia ushindi wa mabao 3-0 ambao Simba ilipata jana dhidi ya Mbao Fc, Aussems alisema wamedhamiria kuhakikisha wanashinda kila mchezo ili waweze kutetea ubingwa hivyo ushindi huo unaendelea kuweka hai mipango yao

"Kila mechi tunacheza kushinda, hata huu mchezo tulistahili kushinda, tulianza kushambulia tangu mwanzo hadi mwisho, mchezo ulikuwa mgumu lakini tulitengeneza nafasi"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
6h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’