Mfanyabiashara Mohammed Dewji 'MO' amefanikiwa kushinda zabuni ya kuwekeza ndani ya klabu ya Simba.
Mwenyekiti wa Kamati ya kusimamia mchakato wa kumsaka mwekezaji wa klabu hiyo, Jaji Mstaafu wa Mahakama Kuu, Thomas Mihayo, alisema Dewji ametimiza vigezo na sifa zote zilizowekwa na kamati yake kwa mshindi wa nafasi hiyo.
"Kamati iliunda kamati ya tathmini ambayo ilikuwa na jukumu la kuthibitisha kama kweli muombaji anakidhi vigezo.
Baada ya muwekezaji kuwasilisha vielelezo vyote vilivyohitajiwa, kamati ya tathmini ilirudisha majibu kwetu kwamba mwekezaji ametimiza vigezo. Hivyo nichukue fursa hii kumtangaza Mohammed Dewji kama mwekezaji mwenza wa klabu ya Simba," alisema Jaji Mihayo.
Baada ya mwekezaji huyo kupatikana Simba inatarajiwa kufanya mabadiliko katika kamati yake ya utendaji ambapo sasa wajumbe watano watalazimika kukaa kando kupisha mabadiliko yatakayofanyika baada ya klabu hiyo kuingia katika mfumo wa hisa.
Kaimu Rais wa Simba, Dokta Salim Abdallah alisema, baada ya kamati ya zabuni kumtangaza mshindi wa mchakato wa uwekezaji wa klabu hiyo, wajumbe watano wa kamati ya utendaji watapunguzwa ili kubakia na saba ambao wataingia kwenye bodi itakayoundwa.
"Baada ya kamati ya zabuni kumtangaza mshindi, kamati ya utendaji itaanza kazi mara moja kutangaza wajumbe saba ambao wataungana na wajumbe saba upande wa mwekezaji, kuunda bodi ya kusimamia klabu yetu," alisema Abdallah.
"Wajumbe wa kamati ya utendaji wapo 12 ambao hawawezi kuingia wote kwenye bodi hivyo baadhi yetu hawatopata nafasi ya kuingia."

ADVERTISE HERE