Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema anatarajia kufanya mabadiliko ya kikosi chake kitakachoikabili Mbao Fc leo kwenye mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Akizungumza baada ya mazoezi yaliyofanyika kwenye uwanja wa Jamhuri, Aussems amesema atawapa mapumziko baadhi ya wachezaji waliokuwa na majukumu ya timu za Taifa
Wakati mlinda lango namba moja Aishi Manula akitarajiwa kukosekana kutokana na kukabiliwa na majeraha ya kiganja cha mkono, Aussems amesema Mganda Emmanuel Okwi na Clatous Chama hawatakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Mbao Fc leo
Katika hatua nyingine Aussems ameridhishwa na ukarabati uliofanywa kwenye uwanja wa Jamhuri
Mchezo dhidi ya Mbao Fc una umuhimu wa kipekee kwa Simba, kwanza mabingwa hao wa Tanzania Bara wanataka kulipa kisasi baada ya kupoteza mchezo wa duru ya kwanza
Pili ushindi utaifanya Simba iandike rekodi mpya ya kushinda michezo 10 mfululizo katika ligi kuu ya Tanzania Bara