Tayari Wajumbe wa Mkutano Mkuu wako ndani, ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam kwa ajili ya kuhitimisha mchakato wa mzabuni wa klabu ya Simba.
Aliyeshinda zabuni atakabidhiwa leo klabu Simba ambapo atamiliki asilimia 50 ya hisa huku asilimia 10 zikitarajia kugawiwa kwa wanachama hai na nyingine 40 kuuzwa kwa wanachama.
Tayari mfanyabiashara na mfadhili wa Simba Mohamed Dewji aliwahi kuonyesha nia ya kuwekeza iwapo tu atapewa asilimia 50 ya hisa, ingawa hata hivyo, leo itajulikana kama atakuwa yeye au wengine kutokana na vigezo vilivyokuwa vimewekwa.
Katika hatua nyingine serikali kupitia Baraza la Michezo la Taifa (BMT) limefanya marekebisho ya kanuni zake na juzi kutoa waraka kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unaotoa maelekezo ya ununuaji na uuzwaji wa hisa za klabu au Chama cha Michezo.
Marekebisho yaliyopo ni kwamba Vyama au klabu zilizoanzishwa na wanachama vikiamua kuuza hisa zake vinapaswa kutenga asilimia 51 kwa ajili ya wanachama na asilimia 49 kwa wanaotaka kununua.
Pia, wanatakiwa kupitia kwenye mamlaka ya mitaji na masoko ili kuidhinishwa na baadaye kurudi kwenye soko la hisa ili kufuata taratibu za uuzwaji na ununuaji.

ADVERTISE HERE