Msafara wa kikosi cha Simba umewasili salama mkoani Morogoro ambako keshokutwa Jumapili kikosi kitachuana na Mbao Fc katika mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Mapokezi ya Simba yaliongozwa na viongozi waaandamizi wa klabu hiyo mkoani Morogoro huku shangwe kubwa likiangushwa na mashabiki wakati basi la Simba likiingia mkoani humo
Simba itaweka makazi yake mkoani Morogoro kwa muda kwani itautumia uwanja wa Jamhuri kwa baadhi ya michezo yake wakati uwanja wa Taifa utakapokuwa umefungwa kupisha michuano ya AFCON U17 inayoanza April 14-28 2019


ADVERTISE HERE