TFF yasisitiza, Amunike hataondolewa Stars

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Mar 2019
TFF yasisitiza, Amunike hataondolewa Stars

Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kocha Emmanuel Amunike ataendelea kuifundisha timu hiyo kwa tofauti na maoni ya wadau mbalimbali ambao wametaka kocha huyo kubadilishwa.

Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Ammy Ninje amesema kuwa malengo waliyompa Amunike ya kuhakikisha timu hiyo katika fainali za Afrika mwaka huu (Afcon) yametimia na hakuna haja ya kumbadili kocha huyo.

Ninje alisema kuwa suala la kocha kubadilishwa halina nafasi katika kipindi hiki kwani TFF na wadau wengi wa soka nchini wamefarijika baada ya kufuzu katika fainali za Afcon kwa mara ya kwanza kwa kipindi cha miaka 39.

Alisema kuwa kwa sasa TFF inajipanga kuona jinsi gani kocha huyo anaiandaa timu hiyo ili kufanya vyema katika mashindano ya hayo yaliyopangwa kufanyika nchini Misri kuanzia Juni 21 mpaka Julai 19.

"Mimi nimeshangazwa sana na mihamko kwenye mitandao ya kijamii. Sijui wanaotaka Amunike aondolewe wametumia vigezo gani. Sababu zao hazina mashiko na sisi tunaendelea naye mpaka katika fainali ya mashindano ya Afcon," alisema Ninje.

Alisema kuwa mjadala huo hauna tija kwa maendeleo ya soka nchini kwani nchi yetu imeshuhudia makocha wengi kutoka katika mataifa tofauti wakishindwa kufikia hatua ambayo Amunike ametufikisha kwa sasa.

"Lazima tujivunie kupata mafanikio haya. Malengo yetu yametimia, sasa sijui baadhi ya Watanzania wanataka nini katika masuala ya soka. Imenishangaza sana, lakini sisi hatufanyi kazi kwa kupitia mihamko ya watu, ushahidi upo wa Amunike alichokifanya," alisema.

Alisema kuwa mpango wa TFF kwa sasa kuhakikisha timu inaandaliwa kwa umakini zaidi na hawafikirii kuongeza wachezaji.

"Kama tutaongeza wachezaji, basi ni wachache sana, maana mpira wa miguu una mambo mengi mbali ya majeraha," alisema Ninje.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’