Simba tayari kuifuata Mbao Fc Morogoro

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Mar 2019
Simba tayari kuifuata Mbao Fc Morogoro

Mabingwa watetezi ligi kuu ya Tanzania Bara Simba kesho Ijumaa wanaelekea mkoani Morogoro tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Mbao Fc

Mchezo huo utapigwa siku ya Jumapili, March 31 katika uwanja wa Jamhuri

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wamedhamiria kutetea ubingwa wao, hivyo wanahitaji kushinda mchezo huo

"Tulipoteza mechi ya kwanza na Mbao Mwanza na sasa tumejipanga kuchukua pointi hizo tatu na kuhakikisha tunaanza kuutumia vyema uwanja wetu wa Jamhuri ambao tunaanza nao katika mchezo huo," amesema Aussems

Hata hivyo licha maboresho yaliyofanywa, uwanja wa Jamhuri bado hauko katika kiwango bora, hali itakayomfanya Aussems alazimike kubadili mbinu ili kwendana na hali ya uwanja huo

"Kutumia Uwanja wa Jamhuri kama nyumbani hatuna jinsi, kutokana na tayari uwanja wa Taifa umefungwa, lakini kuna tofauti kubwa kati ya viwanja hivi"

"Tutajiandaa kucheza kufuatana na hali ya uwanja, muhimu tunahitaji ushindi"

Aussems amesema kikosi chake kitafanya mazoezi kwenye uwanja wa Jamhuri kesho jioni na pengine Jumamosi asubuhi kabla ya kuikabili Mbao Fc Jumapili

Simba inashika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 54, huku ikiwa na michezo nane kibindoni

Hesabu za kutetea ubingwa kwa kocha Aussems zinakwenda sawa mpaka sasa kwani kama Simba itashinda michezo yake yote ya viporo, itaizidi Yanga inayoongoza ligi hiyo kwa alama nane

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’