Simba yapania kumaliza mchezo dhidi ya Mazembe uwanja wa Taifa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Mar 2019
Simba yapania kumaliza mchezo dhidi ya Mazembe uwanja wa Taifa

Kikosi cha Simba kinaendelea na maandalizi kuelekea mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mbao Fc utakaopigwa mkoani Morogoro Jumapili huku kocha Patrick Aussems akiupigia hesabu mchezo wa kwanza wa robo fainali ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa April 06 kwenye dimba la Taifa

Aussems ameweka wazi kuwa Simba ina nafasi ya kutinga nusu fainali ya ligi ya mabingwa lakini ni lazima wapate matokeo mazuri nyumbani kabla ya kuelekea nchini Congo kwa ajili ya mchezo wa marudiano

Kama ilivyo kwa Simba, TP Mazembe nayo ina rekodi ya kipekee inapocheza kwenye uwanja wake

Katika michezo nane iliyocheza nyumbani kwenye michuano ya ligi ya mabingwa, TP Mazembe imeshinda yote bila ya kuruhusu bao hata moja

Ni timu ambayo mara nyingi ushindi wake huupatia nyumbani zaidi kuliko ugenini

"Tunajiandaa kikamilifu, lakini kwa sasa maandalizi yetu tumeyaelekeza zaidi kuelekea mchezo dhidi ya Mbao Fc, amesema Aussems"

"Hata hivyo tayari tunazo taarifa kuhusu wapinzani wetu, muhimu tutahakikisha tunapata matokeo mazuri nyumbani kwani tunafahamu mchezo wa Lubumbashi hautakuwa mwepesi"

"Tutautumia mchezo wetu wa nyumbani kujiwekea mazingira mazuri ya kusonga mbele"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
Simba kuanza na Pirates nyumbani makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
Simba uso kwa uso na Berkane, Pirates kundi C
7h ago
READ MORE β†’
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
Simba yatangaza ratiba ya uchaguzi, Wanachama kuanza kuchukua fomu Oktoba 30
8h ago
READ MORE β†’
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
Hakuna rekodi ya zamani ambayo itaishi mbele ya Simba - Ahmed
11h ago
READ MORE β†’
Makundi CAFCL kujulikana leo
Makundi CAFCL kujulikana leo
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
16h ago
READ MORE β†’
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
1d ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1d ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1d ago
READ MORE β†’