Baada ya kumaliza majukumu ya timu za Taifa, baadhi ya wachezaji 'maproo' wamejiunga na wenzao wanaoendelea na maandalizi ya mchezo dhidi ya Mbao Fc
Nahodha John Bocco, Erasto Nyoni na Aishi Manula leo wamehudhuria mazoezi ya asubuhi yaliyofanyika uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es salaam
Hata hivyo Manula alishindwa kufanya mazoezi kutokana na majeraha ya kiganja cha mkono aliyopata kwenye mchezo dhidi ya Uganda
Mganda Juuko Murshid naye ameripoti mazoezini leo akiwa mchezaji pekee aliyewahi miongoni mwa wachezaji wa kigeni
Wachezaji wengine Emmanuel Okwi, Clatous Chama na Meddie Kagere huenda wakaripoti kambini kesho
Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuelekea mkoani Morogoro keshokutwa Ijumaa tayari kwa mchezo dhidi ya Mbao Fc utakaopigwa katika uwanja wa Jamhuri, Jumapili March 31 2019