Kikosi cha Simba kimerejea 'mzigoni' baada ya mapumziko ya siku kadhaa kwa wachezaji ambao hawakuwa na majukumu ya timu ya Taifa
Simba inajifua katika uwanja wa Boko Veterans jijini Dar es salaam kabla ya kuelekea mkoani Morogoro keshokutwa Ijumaa tayari kuikabili Mbao Fc siku ya Jumapili katika mchezo wa ligi kuu utakaopigwa uwanja wa Jamhuri
Kocha wa mabingwa hao wa Tanzania Bara Patrick Aussems amesema mazoezi anayowapa wachezaji wake yatawasaidia kurejea kwenye ubora wao kwa haraka baada ya mapumziko wakitoka kucheza michezo mfululizo
Lakini pia amesema anahitaji siku kadhaa za kufanya mazoezi kwenye uwanja wa Jamhuri ili kuweza kuuzoea kwani anafahamu mazingira ya uwanja huo si rafiki kwa aina ya mchezo wa Simba
"Tumeamua kuanza mapema ili tupate muda mrefu pia wa kwenda Morogoro kufanya mazoezi katika Uwanja wa Jamhuri ambao kwa namna furani siyo rafiki sana kwetu," amesema Aussems.
Baada ya mchezo dhidi ya Mbao Fc Jumapili, Simba itaendelea kubaki mkoani Morogoro kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya TP Mazembe utakaopigwa April 05 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam