Mchezo wa ligi kuu ya Tanzania Bara kati ya Simba dhidi ya JKT Tanzania uliopangwa kupigwa April 03 2019 huenda ukaahirishwa kupisha maandalizi ya kikosi cha Simba kuelekea mchezo dhidi ya TP Mazembe
Simba itachuana na TP Mazembe April 05 katika mchezo wa kwanza wa robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa utakaopigwa uwanja wa Taifa
Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema tayari wameiandikia barua Bodi ya Ligi kuomba baadhi ya michezo yao kusogezwa mbele, ikiwamo ya April 3, 6 na 12, mwaka huu ili kutumia muda huo kwa ajili ya maandalizi ya mechi dhidi ya TP Mazembe.
Simba ilipaswa kuchuana na KMC April 06, hata hivyo ni wazi mchezo huo hauwezi kuwepo kutokana na kuingiliana na ratiba ya michuano ya ligi ya mabingwa
April 12 pia Simba itakuwa Lubumbashi DR Congo kurudiana na TP Mazembe
Mwishoni mwa wiki hii March 31 Simba itachuana na Mbao Fc katika mchezo pekee kabla ya kuwakabili TP Mazembe