Baada ya kufurahishwa na mafanikio ya kutinga fainali za AFCON 2019, Rais Dk John Magufuli ametoa zawadi ya viwanja vya kujenga nyumba kwa wachezaji wote wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' pamoja na bondia Hassani Mwakinyo
Rais amemuagiza Waziri Mkuu kusimamia agizo hilo kwa kutafuta eneo zuri mkoani Dodoma
Wadau wa soka nchini wamempongeza Rais Magufuli kwa kutambua mchango wa wachezaji hao waliopeperusha vyema bendera ya Tanzania, hata hivyo wamelikumbusha shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) kuhakikisha beki wa Simba Shomari Kapombe anajumuishwa kuwa miongoni mwa watakaopatiwa viwanja hivyo kwa kuwa aliumia wakati akiitumikia timu ya Taifa
Kapombe aliumia kwenye kambi ya Stars iliyokuwa Afrika Kusini mwishoni mwa mwaka jana wakati timu hiyo ikijiandaa na mchezo dhidi ya Lesotho
Tangu wakati huo Kapombe amekuwa nje ya uwanja akitarajiwa kuanza mazoezi mepesi wiki hii
