Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania Mbwana Samatta amesema ushindi wa mabao 3-0 iliyopata Stars jana dhidi ya Uganda umetokana na juhudi zilizofanywa na benchi la ufundi, wachezaji na mashabiki waliojitokeza kwa wingi kuishangia timu
Samatta aliyehusika kutengeneza bao la pili lililowekwa kambani kwa mkwaju wa penati na Erasto Nyoni, amesema anajivunia kuwa nahodha wa Stars iliyokuwa bora sana kwenye mchezo wa jana
"Najivunia ubora uliooneshwa na wachezaji wenzangu,najivunia uwepo wa benchi la ufundi likiongozwa na kocha amunike, najivunia uwepo wa mashabiki waliojitokeza kutusapoti katika mchezo wetu wa jana na najivunia kuwa mtanzania na kapteni wa timu yangu ya taifa", amesema Samatta
"Asanteni wote mliohamasisha na wote mliojotokeza kutusapoti"
Matokeo ya jana yameiwezesha Stars kukata tiketi ya kushiriki fainali za AFCON 2019 ikiwa ni mara yake ya pili tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo mwaka 1957
Nahodha wa kikosi cha Simba John Bocco alikuwa na mchango mkubwa kwenye mchezo huo akitoa pasi za mabao yote mawili.
Bocco alipigiwa kura kuwa nyota wa mchezo huo