Samatta aahidi kuibeba Stars leo

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Mar 2019
Samatta aahidi kuibeba Stars leo

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samatta amesema wachezaji wa timu hiyo leo wana kazi moja tu ya kuhakikisha wanapata ushindi dhidi ya Uganda kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za michuano ya AFCON 2019

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji baada ya kutembelewa na Waziri Mkuu katika kambi ya kikosi cha Stars, Samatta amesema wanajiona kuwa na deni kubwa kwa Watanzania na watahakikisha wanawapa furaha kwa kupata ushindi leo

"Naona naenda kuiongoza nchi siku ya kesho (leo), sitakuwa nahodha kwa ajili ya wachezaji peke yake bali nitakuwa nahodha kwa ajili ya wananchi wote wa Tanzania," amesema Samatta

"Wachezaji wote wako tayari kwa ajili ya kuitetea nchi yao, lengo kubwa ni kuhakikisha bendera yetu ya Tanzania inasimama, Dunia itambue na Afrika yote ifahamu"

Jana Waziri Mkuu Mh Kassim Majaliwa alitembelea kambi ya wachezaji wa timu ya Taifa na kuwaeleza kwamba Serikali na wananchi wanamatumaini makubwa kwa timu yao, hivyo wahakikishe wanapata ushindi katika mechi yao dhidi ya timu ya Taifa ya Uganda leo

"Macho yote ya Watanzania yameelekezwa katika mechi ya kesho (leo) na Serikali inamatumaini makubwa na timu ya Taifa, hivyo muelewe kwamba kesho (leo) ni siku muhimu sana. Lengo letu ni kufikia hatua ambayo mataifa mengine yamefikia"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’