Zana atumia mapumziko kurudi kwao

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
23 Mar 2019
Zana atumia mapumziko kurudi kwao

Baada ya mchezo dhidi ya Ruvu Shooting, wachezaji wa Simba ambao hawakuitwa katika timu za Taifa walipewa mapumziko ya siku tano

Mlinzi wa pembeni Zana Coulibaly alitumia mapumziko hayo kurudi kwao Burkina Faso kuiona familia yake

Zana aliyetua Simba wakati wa usajili wa dirisha dogo mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka 2018, amesema hakuwa amerejea kwao tangu alipojiunga na Simba

Baada ya kuanza kwa kusuasua katika kikosi cha Simba, Zana ameimarisha kiwango chake sasa akiwa mmoja wa wachezaji wa kutegemewa wa mabingwa hao wa soka Tanzania Bara

Zana amempiku Mghana Nicolas Gyan katika nafasi ya ulinzi wa kulia wakati huu ambao mwenye namba yake Shomari Kapombe akiendelea kuuguza majeraha ya goti aliyopata mwishoni mwa mwaka jana wakati akiitumikia timu ya Taifa

Zana anatarajiwa kurejea nchini kesho Jumapili tayari kuanza mazoezi kwa ajili ya maandalizi ya mchezo dhidi ya TP Mazembe

Simba inatarajiwa kuanza kujifua Jumatatu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
6h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
9h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
11h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’