Simba imemualika Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe katika mkutano mkuu wa wanachama utakaofanyika kesho Jumapili, Disemba 03 kuanzia Saa 4:00 asubuhi kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere, Dar es Salaam.
Jana Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Hajji Manara alisema wanataka kuutumia mkutano huo kumtangaza mshindi wa zabuni ya uwekezaji katika klabu ya Simba.
Miezi miwili iliyopita klabu hiyo ilitangaza zabuni kwa wanachama wenye uwezo na mtaji kuanzia Sh. Bilioni 20 kujitokeza na kufanya uwekezaji katika klabu hiyo katika mchakato wa mabadiliko ya muundo wa uendeshaji hadi kuwa wa hisa.
Tajiri na mdhamini wa Simba, Mohammed Dewji 'MO' anatajwa kushinda zabuni hiyo na huenda akatangazwa rasmi kuwa mzabuni wa klabu ya Simba

ADVERTISE HERE