Hatuihofii TP Mazembe - Kagere

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
22 Mar 2019
Hatuihofii TP Mazembe - Kagere

Kinara wa mabao wa kikosi cha Simba Meddie Kagere amesema kwa hatua waliyofikia, wako tayari kucheza na timu yoyote na hawaihofii TP Mazembe watakayochuana nayo katika hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Simba ilipangwa kuchuana na mabingwa mara tano Afrika TP Mazembe katika droo iliyofanyika juzi nchini Misri

Mazembe wanatarajiwa kuja 'machinjioni' uwanja wa Taifa April 05 au 06 kuikabili Simba kabla ya mabingwa hao wa Tanzania Bara kuelekea Lubumbashi kwa ajili ya mchezo wa marudiano utakaopigwa April 12 au 13

Kagere amesema licha ya TP Mazembe kuwa miongoni mwa timu kubwa barani Afrika, lakini Simba sio timu ya kubeza kutokana na mafanikio waliyopata katika michuano hiyo msimu huu

"Tunajipanga kuwakabili. Hatua hii hakuna timu nyepesi na wala hakuna timu yenye uhakika wa kusonga mbele kabla ya dakika 90," amesema Kagere.

Aidha Kagere amesema wanajivunia sapoti ya mashabiki wa Simba wanapocheza kwenye uwanja wa Taifa.

"Ushindi tunaoupata kwenye michezo yetu ya nyumbani unachangiwa pia na mashabiki wetu kwa hamasa kubwa wanayotupa. Tunawaomba waendelee kutusapoti na kutupa hamasa kwenye mchezo huo"

Kagere amekuwa na mafanikio makubwa katika kikosi cha Simba msimu huu akiwa kinara wa upachikaji mabao kwenye michuano yote.

Kwenye hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa Kagere amefunga mabao matatu huku akiwa amepachika mabao 13 katika ligi kuu ya Tanzania Bara

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’