Manara ataka shangwe la Simba lihamie Stars

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
21 Mar 2019
Manara ataka shangwe la Simba lihamie Stars

Afisa Habari wa Simba Haji Manara amewataka mashabiki wa timu hiyo kupeleka shangwe kwa timu ya Taifa siku ya Jumapili itakapochuana na Uganda Cranes katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019

Manara amesema ni zamu ya Stars kufuzu kwa fainali za AFCON 2019 baada ya kujaribu bila ya mafanikio kwa miaka 39.

Amewataka mashabiki wa soka nchini bila ya kujali timu zao, waungane kuipa nguvu Stars ili iweze kupata ushindi dhidi ya Uganda

Naye Mkuu wa Dar es salaam Mh Paul Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya uhamasishaji, amesema jukumu lake kubwa ambalo anaamini amelitekeleza ni kuiweka timu ya Taifa mikononi mwa Watanzania kuelekea mchezo dhidi ya Uganda

Akizungumza na Wanahabari kwenye ukumbi wa mikutano wa kimataifa wa Mwalimu Nyerere leo, Makonda amesema Watanzania wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa Jumapili

Amesema atahakikisha usafiri wa kutosha unakuwepo kutoka kila pembe ya jiji la Dar es salaam

"Daladala yoyote kutoka sehemu yoyote ya jiji la Dar es salaam, nawapa ruhusa ya kuendesha route ya kutoka popote walipo kwenda Uwanja wa Taifa. Ukipata shida yoyote njiani nitafute mimi," amesema Makonda ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama wa jiji la Dar es salaam

"Tukishinda hii mechi nitakahikikisha tunafanya party kubwa sana ndani ya hili jiji la Dar na Tanzania kwa ujumla"

Mgeni rasmi wa mchezo huo atakuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Kassim Majaliwa

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’