Watanzania tunayo kila sababu ya kuiunga mkono timu yetu ya Taifa siku ya Jumapili March 24 2019 itakapochuana na Uganda katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019
Licha ya kushika nafasi ya tatu ikiwa na alama tano kwenye msimamo wa kundi L, Stars inahitaji kuifunga Uganda ili kuwa katika nafasi nzuri ya kufuzu kwani halitakuwa jambo jepesi kwa Lesotho kupata ushindi ugenini dhidi ya Cape Verde ambayo pia inahitaji ushindi ili kuweka hai matumaini ya kufuzu kama Stars haitashinda
Baada ya kusubiri kwa miaka 39, Stars inayo nafasi ya kuweza kuandika Historia ya kurejea katika fainali za michuano hiyo zitakazofanyika huko Misri mwaka huu
Ni kwa buku mbili tu mashabiki wataweza kuushuhudia mchezo huo utakaopigwa uwanja wa Taifa
Mwishoni mwa wiki Simba iliweza kuandika historia ya kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, mashabiki wameaswa kujitokeza kwa wingi Jumapili kama ilivyokuwa kwa Simba, kwani hakuna jambo lisilowezekana