FT : Simba 2-0 Ruvu Shooting

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Mar 2019
FT : Simba 2-0 Ruvu Shooting

Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wameendeleza wimbi la ushindi katika ligi baada ya leo kuibamiza Ruvu Shooting mabao 2-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Taifa

Mabao ya Simba yalipatikana kwenye kipindi cha pili yakiwekwa kambani na beki Paul Bukaba (51') huku bao la pili likifungwa na Meddie Kagere kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 55 baada ya Adam Salamba kufanyiwa madhambi ndani ya eneo la hatari

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems alifanya mabadiliko makubwa ya kikosi chake leo akiwapumzisha baadhi ya nyota waliocheza mchezo wa ligi ya mabingwa mwishoni mwa wiki

Aidha bao alilofunga Kagere leo limemfanya afikishe mabao 13 sasa akishika nafasi ya pili nyuma ya Salim Aiyee wa Mwadui Fc mwenye mabao 16

Simba inaendelea kushika nafasi ya tatu ikiwa imefikisha alama 54, alama tano nyuma ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili huku Yanga ikiongoza ikiwa na alama 67

Hata hivyo Azam Fc na Yanga zimecheza michezo saba zaidi ya Simba

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’