Tutacheza fainali ya ligi ya mabingwa - Niyonzima

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
19 Mar 2019
Tutacheza fainali ya ligi ya mabingwa - Niyonzima

Kiungo Haruna Niyonzima amesema Jumamosi ya March 16 2019 ilikuwa siku ya kipekee kwake na klabu ya Simba baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Niyonzima anayetajwa kuwa nyota wa mchezo wa siku hiyo ambao Simba iliilaza AS Vita Club mabao 2-1, amefichua kuwa licha ya kupata majeraha punde tu baada ya kuingia kuchukua nafasi ya Emmanuel Okwi katika dakika ya 58, amesema alilazimika kuvumilia na kuhakikisha anaitumia vyema nafasi aliyopewa na kocha Patrick Aussems

"Nilijipa moyo na kusema siwezi kuruhusu majeraha haya yakanifanya nitoke nje. Nimekuwa nikijituma ili nipate nafasi kama hii," amesema Niyonzima

"Tangu nikiwa mdogo nimekuwa na ndoto ya kucheza fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika. Hakuna kitakachonizuia kutimiza ndoto hiyo na pia sikuwa tayari kuwaangusha mashabiki wa Simba na Watanzania pamoja na ndugu zangu Wanyarwanda"

"Tuna nafasi ya kucheza fainali ya ligi ya mabingwa mwaka huu, bila shaka tutaweza kwani tuna kikosi cha kufanikisha hilo pamoja na mashabiki wanaotuunga mkono muda wote"

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
24m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’