Droo ya hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika itafanyika keshokutwa Jumatano, March 20 huko jiji la Cairo nchini Misri
Simba pamoja na timu nyingine saba zilizotinga hatua hiyo, zitapangiwa ratiba ya kusaka tiketi ya kutinga nusu fainali
Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema kikosi chake kiko tayari kukabiliana na timu yoyote watakayopangwa nayo.
Amesema wanataka kuendelea kuvunja rekodi kwa kutinga nusu fainali ya michuano hiyo
Timu zilizotinga hatua hiyo ni Simba, Horoya, Al Ahly, Mamelodi Sundowns, Esperance, TP Mazembe, Wydad AC na CS Constantine
ADVERTISE HERE