Try Again ataja kilichoibeba Simba ligi ya mabingwa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
18 Mar 2019
Try Again ataja kilichoibeba Simba ligi ya mabingwa

Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Salim Abdallah 'Try Again' amesema ahadi walizozitoa kwa wachezaji wao pamoja na maandalizi kambambe vimechangia kuibeba timu hiyo kutinga robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Simba iliweka rekodi kwa mara nyingine tena kutinga robo fainali baada ya kuwalaza AS Vita ya DR Congo kwa mabao 2-1, Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam juzi.

"Viongozi tulishikamana. Awali tulikuwa na malengo ya kufika makundi lakini tulivyoona tuna timu nzuri tulikaa chini na kuweka mikakati ya namna ya kuvuka hatua hiyo.

"Hakuna kingine zaidi ya maandalizi mazuri pamoja na ahadi mbalimbali kwa wachezaji wetu, vyote hivyo vimeifanya leo hii Simba kuipeperusha vema bendera ya nchi yetu kimataifa," alisema Try Again.

Kaimu Rais huyo wa zamani wa Simba alisema kinachofuata kwa sasa ni wao viongozi kusubiri marejesho ya Kocha baada ya kusonga mbele ili kuona kwa namna gani wafanye vizuri.

"Kila kitu kipo mikononi mwa kocha wetu. Mwanzo alitaka michezo mingi ya kirafiki tulifavyo hivyo ili kutekeleza matakwa yake," alisema.

Try Again alitoa shukrani zake za dhati kwa wapenzi na mashabiki wa timu hiyo ambao walikuwa wakiisapoti timu hiyo tangu ilipoanza harakati ya kupigania nafasi ya kuingia hatua ya makundi ya michuani hiyo mikubwa Afrika ngazi ya klabu.

Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
2h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
14h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
20h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
23h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’