Baada ya juzi Simba kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Jumamosi ijayo timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' nayo itakuwa dimbani kuikabili Uganda katika mchezo wa kusaka tiketi ya kutinga fainali za AFCON 2019
Jana Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Wallace Karia alitoa pongezi kwa wachezaji, viongozi na mashabiki wa Simba kwa kufanikiwa kuipeleka Simba hatua ya robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa
Karia alisema Stars nayo ina kila sababu ya kufuata walimopita Simba ili kuifunga Uganda Cranes Jumamosi na kukata tiketi ya kutinga AFCON ikitegemea na matokeo ya mchezo kati ya Cape Verde dhidi ya Lesotho
Leo Mwenyekiti wa Kamati ya saidia Stars ishinde Mh Paul Makonda anatarajiwa kuzungumza na waandishi wa habari kuweka hadharani mikakati ya ushindi kuelekea mchezo huo utakaopigwa katika dimba la Taifa
