Baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba wamejihakikishia kuvuna kitita cha zaidi ya Tsh Bilioni 1.5
Kulingana na zawadi zinazotolewa na waandaaji wa mashindano hayo (CAF), timu zote nane zilizotinga robo fainali zitavuna kiasi hicho cha pesa
Aidha kama Simba itatinga nusu fainali itaongeza dau hilo na kufikia karibu Bilioni 1.9, na ikifanikiwa kutinga fainali itavuna zaidi ya Bili 2.9
Bingwa wa michuano hiyo mwaka huu atavuna zaidi ya Tsh Bilioni 5
Droo ya hatua ya robo fainali itafanyika Jumatano, Match 20 2019 katika jiji la Cairo nchini Misri ambapo michezo ya duru ya kwanza ya robo fainali itapigwa kati ya April 5-6 2019 huku michezo ya marudiano ikipigwa kati ya April 12-13 2019