Mwekezaji wa klabu ya Simba Bilionea Mohammed Dewji 'Mo' leo alikuwa miongoni mwa mashabiki waliotekwa na furaha baada ya Simba kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AS Vita Club
Mo alikuwepo uwanja wa Taifa kuwashuhudia vijana wake wakiandika historia kwenye michuano hiyo kwa mara nyingine
Mpaka sasa Mo ndiye mshindi kwani uwekezaji wake mkubwa alioufanya msimu uliopita matunda yake yameanza kuonekana
Mo amesema mnafanikio haya ya Simba ni ya kujivunia kwa mashabiki wote wa Simba na Watanzania wote kwa ujumla
Amesema ushindi huu ni hatua kuelekea kutwaa ubingwa wa Afrika, malengo ambayo aliyaweka msimu uliopita na anaamini Simba haiko mbali kufikia malengo hayo
ADVERTISE HERE