Baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya AS Vita leo na kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema hawataishia hatua hiyo
Akizungumza baada ya mchezo leo, Aussems amesema malengo waliyojiwekea mwanzoni mwa msimu ilikuwa kutinga hatua ya makundi hata hivyo wamefanikiwa kwenda zaidi ya hapo
Amesema kwa sasa Simba haizungumzwi Tanzania tu bali mafanikio hayo ni ya Afrika Mashariki na Kati
"Kwa Simba, kwa Tanzania na hata kwa Afrika Mashariki hili ni jambo kubwa, sasa tutazungumza kuhusu soka kwa Afrika Mashariki na asante kwa Simba," amesema Aussems
"Lengo ilikuwa kufika hatua ya makundi na nilisema hili kundi lipo wazi na hatutaishia robo fainali tutafanya kila jambo ili kusonga mbele"
Simba inasubiri kupangwa kwa droo ya hatua ya robo fainali ambapo kwenye hatua hiyo michezo miwili itapigwa nyumbani na ugenini kupata timu zitakazotinga nusu fainali