Done! Simba yaunguruma uwanja wa Taifa, yatinga robo fainali kibabe

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Mar 2019
Done! Simba yaunguruma uwanja wa Taifa, yatinga robo fainali kibabe

Ule msemo kuwa Simba haifungiki inapocheza katika dimba la Taifa hata ije FC Barcelona umedhihri kwa mara nyingine leo baada ya mabingwa hao wa nchi kuchomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Vita Club na kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Alikuwa ni Clatous Chama 'Triple C' aliyeipeleka Simba robo fainali kwa kufunga bao safi katika dakika za lala salama

Krosi ya chini ya nahodha John Bocco ilipishana na kiungo Haruna Niyonzima na kumkuta Chama aliyeujaza mpira kimiani upande wa kulia wa mlinda lango wa Vita

AS Vita walitangulia kufunga bao la kuongoza kwenye dakika ya 13 kupitia kwa Kazadi Kasengu kabla Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' hajaisawazishia Simba kwenye dakika ya 33 akimalizia pasi murua iliyopigwa na Mzamiru Yassin

Leo Simba imedhihrisha iko tayari kuchuana na vigogo wa soka barani Afrika ikiwa miongoni mwa timu nane bora zilizotinga robo fainali

Simba imetinga robo fainali ikishika nafasi ya pili kundi D nyuma ya Al Ahly ambayo imeichapa JS Saoura mabao 3-0

Aidha mashabiki nao wametimiza wajibu wao kwa kuujaza uwanja wa Taifa leo. Hakika uzalendo wa mashabiki wa Simba kwa timu yao ni wa kujivunia

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
47m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
8h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’