Unamkumbuka yule 'dogo' ambaye video yake ilisambaa kwenye mitandao ya kijamii akilia baada ya Simba kufungwa mabao 2-0 na JS Saoura? Basi leo amekutanishwa na mchezaji wa ndoto zake, Meddie Kagere
Rackeem amesafiri na wazazi wake kutoka mkoani Tanga kuja jijini Dar es salaam kushuhudia mchezo kati ya Simba dhidi ya AS Vita Club
Shukrani za kipekee ziuendee uongozi wa Simba hasa Afisa wake wa Habari Haji Manara ambaye amefanikisha kupatikana kwa kijana huyo aliyejipachika jina la 'MK 14' kutokana na kumhusudu sana Kagere
Rackeem ataushuhudia mchezo wa leo akiwa jukwaa la watu maarufu (VIP)
ADVERTISE HERE