VIta Club wapagawa, wapiga mwandishi

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Mar 2019
VIta Club wapagawa, wapiga mwandishi

Maafisa wa klabu ya AS Vita wanatuhumiwa kumshambulia mwandishi wa gazeti la Champion, Ibrahim Mussa katika mazoezi ya timu hiyo yaliyofanyika uwanja wa Taifa jana jioni

Tukio hilo la kushambulia mwandishi limelaaniwa vikali na wadau wa soka nchini akiwemo msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara

Manara amesema tukio hilo lisilo la kiungwani linadhihirisha ni kwa kiasi gani timu hiyo imeingia 'mchecheto' kuelekea mchezo baina ya timu hizo jioni ya leo

Manara amewataka mashabiki wa Simba wawe watulivu, wasilipize kisasi na badala yake wajitokeze kwa wingi uwanja wa Taifa kuipa nguvu timu yao iweze kuibuka na ushindi

"Hiki kitendo wa watu wa Vita kumpiga huyu kijana anayeonekana Mwandishi wa Habari siyo cha kiungwana na kinapaswa kilaaniwe," amesema Manara

"Kwanini hawa watu wamepaniki kiwango hiki?"

"Nawasihi Wanasimba msirudishie ugomvi ili wasipate sababu ya kulalamika"

"Twendeni tukamalizane nao kwenye Uwanja pale Taifa usiku wa leo"

Tangu ilipowasili juzi, AS Vita maafisa wa timu hiyo wamegoma kuzungumza na waandishi wa habari huku wakizuia mtu yeyote wakiwemo waandishi kushuhudia mazoezi yao

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’