Kibadeni akumbushia ya mwaka 1993, amtahadharisha Aussems

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Mar 2019
Kibadeni akumbushia ya mwaka 1993, amtahadharisha Aussems

Mwaka 1993 Abdallah Kibaden akiwa kocha wa Simba, aliiongoza timu hiyo kutinga fainali ya kombe la CAF ikikaribia kabisa kutwaa taji hilo baada ya kulazimisha suluhu ya bila kufungana dhidi ya Stella Abidjan katika mchezo wa mkondo wa kwanza uliopigwa Ivory Coast

Ikihitaji ushindi katika mchezo wa pili uliopigwa uwanja wa Uhuru, Simba ilijikuta ikipoteza kwa kufungwa mabao 2-0

Kuelekea mchezo dhidi ya Vita Club kesho, Kibaden amemtahadharisha kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems kuwa ni lazima awajenge wachezaji kisaikolojia ili wahakikishe wanapambana ndani ya dimba kuweza kupata ushindi

"Nakumbuka mwaka 1993 tuliweka kambi Zanzibar, lakini huku nyuma zikaundwa kamati nyingi, walianza kujiandalia sherehe mapema, walishona sare na hata wachezaji wakaaminishwa tayari wamechukua kombe kabla hata ya kucheza," alisema Kibadeni.

"Nina mfano halisi kuhusu mechi za namna hii, wanapojiandaa na mechi na AS Vita ni jambo jema kuwapa hamasa wachezaji lakini wasiaminishwe kuwa watashinda kabla ya kucheza"

Kibadeni amesema wachezaji hawapaswi kwenda uwanjani na matokeo kwa kuwa yanaweza kuwaathiri na wakacheza chini ya kiwango kama ilivyowatokea wao mwaka 1993.

Mchezo dhidi ya As Vita unaopigwa kesho kwenye uwanja wa Taifa, una umuhimu wa kipekee kwa kikosi cha Simba kwani matokeo ya ushindi yatawahakikishia mabingwa hao wa Tanzania Bara kutinga hatua ya robo fainali

Hata hivyo As Vita nao wanahitaji kushinda ili waweze kusonga mbele. Matokeo yoyote tofauti na ushindi kwa timu zote kesho, yatazipa nafasi JS Saoura na Al Ahly kutinga hatua inayofuata

Hii ndio sababu ya mchezo huo kuitwa fainali kwani kila timu inahitaji matokeo ya ushindi tu ili iweze kubaki katika mashindano

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
18m ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
12h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’