Aussems amewapania kwelikweli AS Vita

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Mar 2019
Aussems amewapania kwelikweli AS Vita

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema wanayo kila sababu ya kushinda mchezo wa keshokutwa dhidi ya AS Vita utakaopigwa saa moja usiku katika uwanja wa Taifa

Aussems ambaye msimu huu ameiongoza Simba kwa mafanikio makubwa kwa kuweza kuipeleka hatua ya makundi, amedhamiria kuvuka malengo kwa kutinga robo fainali

"Mchezo huu muhimu kuchezwa katika uwanja wetu wa nyumbani mbele ya mashabiki wetu, inatuongezea kujiamini.

"Tuko katika nafasi nzuri zaidi ya kupata ushindi kuliko wapinzani wetu," amesema Aussems

"Nafahamu mchezo hautakuwa mwepesi kwani wapinzani wetu nao wanahitaji ushindi ili wafuzu"

"Lakini sisi tuna faida ya kupata uungwaji mkono kutoka kwa mashabiki wetu. Ni muhimu mashabiki wakajitokeza kwa wingi uwanjani, wajaze uwanja na watuunge mkono kwa muda wote wa mchezo, ushindi utakuwa upande wetu"

Mshindi wa mchezo kati ya Simba dhidi ya AS Vita atajihakikishia kutinga hatua ya robo fainali na timu itakayoshinda kwenye mchezo kati ya Al Ahly dhidi ya JS Saoura unaopigwa Misri

Matokeo ya sare yatazipa nafasi JS Saoura na Al Ahly kutinga robo fainali

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
5h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
8h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
10h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
15h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’