Niko fiti kuwakabili AS Vita - Wawa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
14 Mar 2019
Niko fiti kuwakabili AS Vita - Wawa

Beki kisiki wa Simba Paschal Serge Wawa amesema yuko imara kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vital utakaopigwa keshokutwa Jumamosi kwenye uwanja wa Taifa

Wawa alipata majeraha ya kifundo cha mguu kwenye mchezo uliopita dhidi ya JS Saoura ambapo Daktari wa Simba Yassin Gembe alisema beki huyo raia wa Ivory Coast pamoja na kiungo Haruna Niyonzima walipata majeraha ya enka kutokana na mazingira ya uwanja wa Agosti 20 ambao una nyasi bandia

Wawa amesema hali yako imeimarika na atacheza mchezo wa Jumamosi

"Niko vizuri sasa, niliumia katika mechi iliyopita kule Algeria, lakini sasa ninaendelea vizuri na nitacheza mechi ya Jumamosi," amesema

"Naamini tutafanya vizuri kwenye mchezo huo, tutapambana kwa sababu tunataka kuwafurahisha mashabiki wetu na vilevile tunataka kuweka rekodi ya kutinga robo fainali"

Wawa alishiriki mazoezi ya Simba yliyofanyika kwenye uwanja wa Boko Veterans jana jioni

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
5h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
17h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
23h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’