Simba yaanza maandalizi ya kuimaliza AS Vita

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
13 Mar 2019
Simba yaanza maandalizi ya kuimaliza AS Vita

Kikosi cha mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba leo kinaanza maandalizi ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita utakaopigwa Jumamosi, March 16 kwenye uwanja wa Taifa

Baada ya kuwasili salama jana kutoka Algeria, wachezaji walipewa mapumziko na leo wataingia kambini leo kujiandaa na mchezo huo ambao Simba inahitaji ushindi ili iweze kutinga robo fainali

Daktari wa kikosi cha Simba Dk Yassin Gembe amesema wachezaji wa timu hiyo wako katika hali nzuri isipokuwa Paschal Wawa na Haruna Niyonzima ambao walipata majeraha madogo kwenye mchezo dhidi ya JS Saoura

Katika hatua nyingine, wachezaji Emmanuel Okwi, Juuko Murshid na Erasto Nyoni leo watajumuika kwenye mazoezi ya Simba ynayofanyika uwanja wa Boko Veterans

Wachezaji hao walikosa safari ya Algeria kutokana na sababu mbalimbali ambapo Juuko alikuwa akitumikia adhabu ya kadi mbili za njano wakati Okwi na Nyoni wakiwa majeruhi

Dk Gembe amesema hali za Okwi na Nyoni zimeimarika na wataanza mazoezi kamili na wenzao leo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
3h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
15h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’