Nahodha wa kikosi cha Simba John Bocco amesema baada ya kurejea kutoka Algeria, mawazo yao yote wameyaelekeza kwenye mchezo wa Jumamosi dhidi ya AS Vita utakaopigwa katika dimba la Taifa
Bocco amesema wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo huo ambao Simba inahitaji matokeo ya ushindi ili kuweza kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
"Tunamshukuru Mungu tumefika salama, tuna mchezo mwingine tutacheza na AS Vita, mimi naamini kabisa kwa morali tuliyonayo na mbinu za kocha tukiwepo nyumbani tutapambana na tutafuzu," amesema Bocco muda mfupi baada ya kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl Julius Nyerere
Simba imetua jioni ya leo Jumanne kutoka nchini Algeria ambako ilikwenda kuchuana na JS Saoura katika mchezo wa raundi ya tano michuano ya ligi ya mabingwa kundi D, mchezo ambao wenyeji walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0