Tutawapa furaha mashabiki uwanja wa Taifa - Wawa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Mar 2019
Tutawapa furaha mashabiki uwanja wa Taifa - Wawa

Baada ya Simba kupoteza mchezo wake wa Ligi ya Mabingwa hatua ya makundi mbele ya JS Saoura, sasa wachezaji wameamua kuhamishia hasira zao kwa wapinzani wao AS Vita ili kushinda na kutinga hatua ya robo fainali.

Kwa sasa kundi D limekaa kimtego kwani hakuna hata mmoja mwenye uhakika wa kutinga hatua ya robo fainali mpaka jumamosi ambapo timu zote nne zitacheza mchezo wa mwisho wa hatua ya makundi.

Al Ahly ambao wana pointi saba watamenyana na JS Saoura ambao kwa sasa ni vinara wakiwa na pointi nane, huku Simba ambao wanaburuza mkia watamenyana na AS Vita ambao wapo nafasi ya tatu wakiwa na pointi saba.

Beki wa Simba mwenye miraba mnne, Pascal Wawa amesema walionyesha juhudi za kupambana kutafuta matokeo kwa manufaa ya timu pamoja na taifa ila bahati haikuwa upande wao mbele ya JS Saoura.

"Tunashukuru kwa sasa, maana tulipambana kutafuta matokeo ila bahati haikuwa yetu kwa sasa hesabu zetu ni mchezo wetu ujao dhidi ya AS Vita ambao tutakuwa nyumbani.

"Bado tuna nafasi ya kurejesha tabasamu kwa mashabiki pamoja na timu kiujumla kwani mchezo wetu mmoja upo mikononi mwetu, ushindani ni mkubwa nasi tutapambana alichopanga Mungu huwezi kupangua," Wawa amenukuliwa na mtandao wa SalehJembe

Simba inatarajiwa kurejea nchini mchana wa leo Jumanne kutokea Algeria na itaelekea moja kwa moja kambini kujiandaa na mchezo dhidi ya AS Vita baada ya kutua uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
2h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
3h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
5h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
9h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
21h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’