Mogella amtaja Okwi kipigo JS Saoura

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Mar 2019
Mogella amtaja Okwi kipigo JS Saoura

Katika mchezo wa juzi, JS Saoura walipata ahueni baada ya kukosekana kwa Mganda Emmanuel Okwi na huenda ndio ikawa sababu iliyofanya safu yao ya ulinzi icheze kwa kujiamini sana baada ya kukosa kashikashi kutoka kwa washambuliaji wa Simba

Mkongwe Zamoyoni Mogella ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Simba, amesema mchezo dhidi ya JS Soaura umedhihirisha umuhimu wa Okwi katika kikosi cha timu hiyo hasa kwa michezo ya ligi ya mabingwa

"Kukosekana kwa Okwi kwenye mchezo dhidi ya JS Saoura kulisababisha safu ya ushambuliaji ya Simba kukosa makali," amesema Mogella

"Ni kweli Kagere ni mpambanaji lakini Okwi ana kipaji cha pekee. Ni mbunifu, 'purukushani' zake ndizo zinazowanufaisha Kagere na Bocco kuweza kufunga kwa urahisi."

Okwi alishindwa kwenda Algeria na kikosi cha Simba kutokana na kusumbuliwa na jeraha la goti alilopata kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Lipuli Fc

Amekuwa nje kwa wiki mbili, bado hatma yake haijafahamika kuelekea mchezo dhidi ya Vita Club

Wachezaji Juuko Murshid na Erasto Nyoni nao hawakusafiri Algeria lakini huenda wakawa tayari kwa mchezo huo wa Jumamosi

Juuko amemaliza adhabu ya kadi mbili za njano wakati Nyoni aliyepona majeraha ya goti hivi karibuni, alipewa muda zaidi wa kufanya mazoezi ili aweze kuwa 'fit'

Kiungo Jonas Mkude yeye atawakosa Vita Club kwa kuwa ana kadi mbili za njano

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8m ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
4h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
16h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
21h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’