Mapema leo Msemaji wa klabu ya Simba Haji Manara alizungumza na waandishi wa habari ambapo ajenda kuu ikiwa ni mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Vita Club utakaopigwa Jumamosi, March 16 kwenye uwanja wa Taifa
Manara alitaja viingilio vya mchezo huo ambapo kiingilio cha chini kabisa ni Tsh 3000/- jukwaa la mzunguuko, VIP A ni Tsh 20,000/-, VIP B ni Tsh 10,000/- huku tiketi maalum za Platinum zikiwa Tsh 100,000/-
Manara aliwataka mashabiki wa Simba kufurika kwa wingi kwenye uwanja wa Taifa ili ikiwezekana kuujaza uwanja huo unaochukua mashabiki takribani elfu 60
Amesema Simba inahitaji sana nguvu ya mashabiki wake kwenye mchezo wa Jumamosi ambao ni lazima mabingwa hao wa Tanzania Bara washinde ili waweze kutinga robo fainali
Tayari uongozi wa Simba umeweka hadharani maeneo ambayo tiketi zitapatikana;

