Baada ya Simba kupoteza mchezo usiku wa kuamkia leo nchini Algeria kwa kufungwa mabao 2-0 na JS Saoura, nafasi pekee iliyobaki kwa mabingwa hao wa nchi ili kuweza kusonga mbele ni ushindi dhidi ya AS Vita Club
Simba bado ina nafasi ya kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa licha ya kushika nafasi ya nne kwenye msimamo wa kundi D ikiwa na alama sita
Mkuu wa Habari na Mawasiliano wa Simba Haji Manara amesema mchezo dhidi ya AS Vita ni zaidi ya kufa au kupona
"Ni zaidi ya Kufa au kupona Kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi ya AS Vita utakaochezwa Taifa Jumamosi ijayo," amesema Manara
"Bila kujali matokeo yatakayotokea Misri baina ya Al Ahly na Soura ambao nao wanacheza siku hiyo ya tarehe 16,ushindi wowote tutakaoupata dhidi ya Wacongo hao tutafuzu kwenda robo fainali"
"Hiyo sio Yes We Can,hiyo ni Do or Die kama ilivyokuwa ulivyokuwa mchezo dhidi ya Nkana Fc"